Header Ads

KAKA NA DADA YANGU ,UNATAKA KUMJUA ANAEKUPENDA KWELI MWENYE NIA YA NDOA NZURI ?? SOMA HAPA ...



 👉Hujitoa Nafsi Yake,Mwili Wake Kwaajili Yako Sio kukupa Pesa Na Vitu Tu Hapana Hivi N Hatua Ya pili Ya Upendo Wa Dhati..

🍞Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

— Yohana 3:16 ,Mungu Alitupenda MPAKA Akaitoa Nafsi Yake Kwaajili Yetu Huu Ndio Upendo...

👉Hutoa Muda Wake hatakama Anakua amebanwaKukutoa Kwenye Shida Flani Au Kukufanya Usahau Mambo Flani Yanayokuumiza.

🍞huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.”

— 1 Petro 5:7 ,Upendo Humfanya MTU Ashughulike Na Mambo Ya Anaempenda Maana Huumia Kama Amiavyo Anaempenda.

👉Ukikosea Huwa Hakuhesabii Makosa Yako Wala Misaada Anayo Kupa Huwa Huiona Nikama Alijifanyia Mwenyewe Huku Sitiri Na Lolote Linalokuja Kwako..

🍞“Heri waliosamehewa makosa yao, Na waliositiriwa dhambi zao.”

— Warumi 4:7

👉Ukimpa Utaratibu Sahihi Wa Kukuoa au Kumuoa Hatakama Mgumu Huufanya Bila Shaka Yaan Hata Ukimwambia Hatutafanya Chochote Hadi Ndoa atafata TUU..

🍞“Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda.”

— Mwanzo 29:20 ,,Yakobo Alitumika Miaka Saba Ilikua N Mali Ya Kumpata Mke Lakini Hakuona Tabu Na akaona Midogo Na hakuwaza KUA Je Nikifa??😂😂Nitakosa Jiko Hapana Hakuwqza Hivyo ....

N.B UPENDO WA DHATI NI HUU...1 Wakorintho 13 (Biblia Takatifu)

¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯

⁴ Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

⁵ haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

⁶ haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

⁷ huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

⁸ Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika...

👆👆👆UKIONA UKO KWENYE MAHUSIANO NA MTU YUKO KINYUME NA HAYA YAAN SIO MVUMILIVU ANATAKA MUANZE KUGUSANA GUSANA HOVYO PIA HAKUAMINI VIZURI NA HANATUMAINI NA UPENDO WAKO NAKADHALIKA AISEE EM MUULIZE MUNGU TENA VIZURI MAANA MKIRUKA UCHUMBA NDOA ITAWASUMBUA....

No comments:

Powered by Blogger.