Header Ads

Umuhimu wa kunywa maji ya dafu kiafya

 

Maji ya madafu ni yamekuwa yakijipatia umaarufu sana katika mikoa ya ukanda ya pwani ya Tanzania.

Lakini licha ya kutumia kinywaji hicho kama kinywaji, pia husaida sana kuondoa kiu, maji ya madafu yana faida lukuki kwa afya ya mwanadamu.

Miongoni mwa faida za maji hayo ni pamoja na kuimarisha misuli na ubongo, huku pia yakitumika kuzuia upungufu wa maji mwilini.

Maji ya madafu yanasaidia kuzuia muonekano wa kizee (anti-aging) hususani pale linapotumika vyema mara kwa mara.

Pia maji ya dafu yanasaidia kuimarisha mfumo wa usagaji chakula tumboni. Maji ya madafu yanasaidia kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili.

Maji ya madafu yanasaidia kukukinga dhidi ya magonjwa ya moyo pamoja na presha.

Hali kadhalika maji ya madafu yana utajiri mkubwa wa virutubisho mbalimbali, huku yakiwa na kiasi kidogo cha kalori

Mbali na hayo, maji ya madafu ni msaada mkubwa katika kuimarisha mzunguko wa damu mwilini.

No comments:

Powered by Blogger.