Header Ads

SMS Za Nguvu Za Kutumia Baada Ya Kupewa Namba Na Mwanamke

 

Tangu tuweke chapisho ambalo linagusia swala la mbinu tofauti tofauti za kuomba namba ya simu ya mwanamke, tumekabiliwa na janga jingine ambalo baadhi wa readers humu ndani wamekuwa wakituandama katika inbox na maswali ya kurudia rudia ya 'Jinsi ya kuufunga mchezo baada ya kupewa namba na mwanamke'

Tumekuwa tukiwajibu baadhi ya readers wetu na tumeamua kuweka wazi mbinu rahisi ambayo itamfunga mwanamke ili uweze kukutana naye mara ya pili, ya tatu, ya nne...

Na kufanikisha hivi, tumekuja na mbinu ambayo kwa kawaida imekuwa ikitumiwa na guru wengi ambao wamebobea katika sekta ya kudeti wanawake.

Zama nami...



Ok. Umefuata mbinu ya moja kwa moja ukamfanya mwanamke akakupatia namba yake ya simu.

Uliongea naye na uliona anavutia kupindukia...

Ulikuwa ama alikuwa na haraka hivyo hukupata nafasi ya kuongea naye kwa muda mrefu bali ulichukua namba yake ya simu.

Sahizi umeachwa hujui ufanye nini!

Je umpigie simu ama umtumie ujumbe mfupi?

Utasema ama utamwambia nini baada ya kuwasiliana naye?

Je, utamuuliza kama atoke deti na wewe au la?

Ok bila kupanic, mbinu ya kufanikisha maswali haya ni rahisi...

Mwanzo ni rahisi kama kusema A...B...C...

SMS za nguvu za kumtumia mwanamke siku ya leo baada ya kukupatia namba
1. Funga deti na yeye
Jambo la kwanza kabisa ambalo unafaa kufanya wakati ambapo atakuachia namba yake ya simu ni uhakikishe ya kuwa unamwomba atoke deti na wewe. Na meseji unayohitajika kumtumia ni kama ifuatayo...

"Hi. nlikuwa nahakikisha kama umefika nyumbani salama. Nimefurahia sana kukutana na wewe. Ningependa tukutane wakati mwingine. Jumamosi nitakuwa free. Nije nikuchukue wakati gani?"

SMS hii huwa inafanya kazi kwa mambo mawili: Jambo na kwanza ni kuwa inamfanya ajihisi yuko salama, yani kujiona ya kuwa kuna mtu anadhamini maslahi yake, jambo ambalo wanawake wengi wanatamani kuwa nalo.

Pili ni kuwa unamlazimisha kujiazima. Aidha akubali kutoka deti na wewe ama kukukataa papo hapo. Kivyovyote vile utaujua msimamo wake.

Kama atakubaliana na wewe na kujibu sms yako,  turuke katika hatua ya pili.

2. Mfunge kwa kumpigia simu
Kabla kutoka deti na yeye lazima ufahamu mambo angalau kidogo kumhusu. Kujua mambo kadhaa kumhusu kutakupa wewe nafasi ya rahisi kuifanya deti yako na yeye kuvutia, bila kuboesha. Pia kumpigia simu kunajenga ile hisia ya mapenzi ambayo hujitokeza katika mazungumzo ya simu.

Pia unataka kumjulisha ya kuwa uko interested na yeye, lakini usiivuke mipaka yako hapa. Meseji ya pili inafaa ienda hivi:

"Poa. Natumai kukutana na wewe hio siku. Nitakupigia simu wakati flani kukujulisha vile tutavyoendelea. Kesho inaweza kuwa siku nzuri kwako?"

 Kutumia meseji hii ina nguvu zifuatazo:  Unaufunga mchezo wako wa simu. Unamwambia ya kuwa deti yenu itafanikiwa. Pia unamwambia ya kuwa unapanga sehemu ambayo unapania kukutana kwa deti. Kiukweli ni kuwa utajua vitu ambayo anapenda wakati ambapo utampigia simu, na hii itakuwa kama msingi wenu wa kwanza katika deti.

Halafu sasa itambidi akujibu. Na hapa ndipo maongezi yenu yataanza kupanda kwa kasi. Haswa kama amependezwa na wewe.

No comments:

Powered by Blogger.