KAMA MWANAUME ANAKUFANYIA MAMBO HAYA MATANO BASI JUA UNADANGWA!
(1) Hataki kukupeleka kwake mechi zote mnachezea kwako; Kama una mwanaume anakuambia anakupenda lakini hajawahi kukupeleka kwake, au unapajua kwake lakini hataki muende, ni karibu tu ila anataka kufanyia mapenzi kwako na mara nyingi akija anakula kabisa na kuondoka, anaweza alete matunda au asilete kitu lakini anakula na hata hajiongezi, hataki mchezee kwake kwani inamaanisha ukienda kwake chakula atanunua yeye na si wewe, huyu Dada ni mdangaji jua kuwa unadangwa.
(2) Ghafla anafukuzwa au kusimamishwa kazi/biashara haziendi vizuri; Mpaka wakati mwingine unajiona una gundu, umekutana naye hata mwezi haujaisha kasimamshwa kazi, kuna matatizo kazini au biashara imesimama, hujawahi muona kazini wala kuiona hiyo biashara lakini ana maneno maneno mengi kisha anakuomba pesa ya kutumia au akaongezee mtaji, dada yangu mwanaume unayekutana naye ghafla anapata matatizo huyo ni mdangaji unadangwa! Alikua hajawahi kukupeleka kazini, hujaiona Biashara yake lakini ghafla kila kitu kinabadilika.
(3) Anakuacha unalipia kila kitu; Mkitoka out, mkienda sehemu na hata wakati mwingine kwenda gest anaenda kukuvunja yeye lakinia nataka ulipie chumba wewe. yaani bili inakuja ukigusa tu pochi ananyamaza au anaenda chooni kabisa akiona bili inakuja. Wengine hata anakuambia tuchangie au sina pesa lipia nitakulipa halafu hatoi. Dada yangu kama umekutana na huyu jua tu unadangwa na hakuna mapenzi hapo!
(4) Anakutambulisha kwao unaanza kubeba matatizo ya familia yao; ghafla kakutambulisha kwao, ndugu zake wamekupokea kwa bashasha mpaka ukasema wakwe si ndiyo hawa. Lakini unshangaa wanaanza kukuomba pesa, yaani kama ushaolewa kwao, kila ukienda wanataka vizawadi na yeye hajali aua nakuambia kabisa wape au kukuambia Mama anashida flani, au sijui hiki sijui kile! Hapa sio kwamba jamaa ni mdhangaji tu lakini dada yangu hapa umekutana na familia ya wadangaji na inawezekana kuna wengine kama kumi wametambulishwa hivyo hivyo na wote mnadangwa!
(5) Anakushirikisha kwenye mambo anayofanya lakini kwa majina yake; Akinunua kiwanja anakuonyesha, gari anakuonyesha, akinunua mapazia hata mpaka kijiko nakuonyesha. Wewe unafurahi na kuona mume huyu, lakini sasa anataka uchangie, anakufanya uhisi kama kile kitu ni henu lakini vyote vina majina yake, tununue gari, tuanze kujenga kwenye kiwanja chetu, tununue mapazia ya pale nyumbani na upuuzi puuzi mwingi. Kila kitu anaweka kwa jina lake na ukimuuliza anakuambia “Inamaana huniamimi, kama hatuaminiani hatujaiana tukioana itakuaje?” Dada yangu uanadangwa!
Huyo mwanaume sio anajifanya kukushirikisha ili uwe rahisi kutoa, mara nyingi ukichunguza utakuta kuna wenzako wawili watatu nao wanampa pesa kama hawana akili nzuri kwakua nao wanaambiwa nyumba yetu, kiwanja chetu, gari letu na ujinga ujinga mwingine wetu! Dada zangu najua nyie ni wagumu sana kuelewa ila endelea kudangwa na siku ukisafishwa kila kitu usisahau kuja na kisa chako ili niwaandikie wenzako namna ulivyotapeliwa ili wajifunze kupitia kwako!
No comments: