Nimechanganyikiwa naomba ushauri
Mimi ni Binti wa miaka 26, sijaolewa lakini nina mchumba wangu ambaye tuko kwenye mahusiano kwa miaka mitano sasa. Nikiwa chuo mwaka wa pili mchumba wangu yeye alikua kazini, alikua badi hajajitambulisha kwetu lakini kwao walikua wananifahamu. Kipindi hicho nakumuka Mama yake alipata ajali, alipooza mwili mzima kuanzia shingo kushuka chini hivyo akawa mtu wa kufanyiwa kila kitu.
Kwakua dada zake walikua makazini mchumba wangu aliniambia niache chuo ili kumhudumia Mama yake, mwanzo nilikataa lakini aliniambia kuwa anaenda kujitambulisha kwetu ingawa hakutaka niwaambie mambo ya kuacha chuo. Kwelia lijitambulisha na kuwaambia kuwa anataka kunioa, Baba yangu alikataa na kumuambia asubiri mpaka nimalize chuo ndiyo tutaoana. Alionekana kuwa siriasi, alitoa mhari yote na kusema atasubiri mpaka nimalize chuo.
Bado alitaka nibaki na Mama yake, ingawa alikua na mfanyakazi lakini walitaka angalau mtu mwingine wafamilia, alinisihi sana akiniambia yule ni Mama yake hivyo ni kama Mama uangu. Nilimkubalia kwa kigezo kuwa niahirishe mwaka mpaka Mama yake atakapojisikia vizuri. Alinikubalia na kweli niliahirisha mwaka na kuanza kumuuguza Mama yake bila kwetu kujua, nimemuuguza Mama yake ni mwaka wa tatu sasa, ndugu zangu wanajua nimeshamaliza chuo na nafanya kazi.
Baada ya ule muda wa kumaliza chuo kufika nilimuambia mambo ya ndoa akasema tusubiri kwanza kwani Mama yake hali ni mbaya akitegamaa tufanye sherehe. Lakini kumekua na vituko vingi, pamoja na mimi kumhudumia Mama yake lakini siishi kumfumania na nikisema anakua mkali. Nikionge habari za ndoa anakua mkali sana na hajali tena pamoja na kusihi na Mama yake, yeye ni kama ana maisha mengine.
Mwezi uliopita Mama yake alifariki dunia, baada ya mazishi baadhi ya ndugu wakamuambia anioe lakini hakutaka. Alijibu kwa dharau kuwa hawezi kuoa wanawake wawili kwani kuna mwanamke mwingine ana mtoto wake na wameshafunga ndoa ya serikali. Nilijikuta nachanganyikiwa kwani nimecha kila kitu kwa ajili yake, nyumbani wanajua nishamaliza chuo nafanya kazi huku chuoni nako nikifuatilia wanasema nimekaa sana siwezi kuendelea kwani niliahirisha mwaka mmoja tu, sasa nashindwa nifanye nini niko njia panda?
No comments: