Header Ads

UNAMLAZIMISHA MUME/MPENZI WAKO KURUDIANA NA X WAKE, SOMA KISA CHA HUYU DADA!

Hakuna kitu ambacho kilikua kinaniuma kama kujua kua mume wangu kila siku anaonana na X wake, ingawa alishaniambia kuwa hana mahusiano naye na hakukua na dalili yoyote ya yeye kunisaliti lakini kile kitendo cha wao kufanya kazi sehemu moja kilinifanya kuchanganyikiwa hasa ikizingatia kuwa waliachana kwa sababu ya dini na si kwakua walikua hawapendani.

Walikua katika mahusiano kwa miaka minne lakini walipofikia kutambulishana ndugu walikataa katakata ikabidi waachane. Hapo ndipo nilipokutana na mume wangu na miezi sita baadaye tulifunga ndoa. Nilikua naumia sana kwani kwa sehemu waliyokua wanafanya kazi hakukua na kuhama, mimi nikiwa Mama wa nyumbani kila siku nilikua naumia kua wanatumia muda wao mwingi pamoja kuliko mimi ninavyotumia muda na mume wangu.

Nilikua nikipiga simu mara kwa mara na kama akichelewa kupokea basi ilikua ni maneno, nikimuona mume wangu online kama hachat na mimi basi napanikia najua wanchat pamoja. Kweli nikikua na wivu na kila mara mume wangu akirudi ulikua ni ugomvi sijui kwanini lakini kila mara nilikua naona kama kakosa tu. Baada ya muda mume wangu alianza kuchelewa kurudi nyumbani, alikua si mlevi lakini alianza kunywa.

Kila siku alikua analalamika kua nina mdomo sana nataka kumtawala na simpi raha, kuna wakati nilikasirika na kumuambia achague mimi au huyo X wake. Alishangaa kwani ni mara kibao alishaniambia kuwa hawako pamoja lakini mimi nilihisi kua wapo pamoja, tulinuniana na aliniambia hajui cha kuchagua kwani hayuko na huyo mwanamke mwingine.

Hakutaka hata kunipeleka katika sherehe za kiofisi kwani kuna wakati alinipeleka tukagombana mbele za watu akaniambia namuaibisha. Kusema kweli nilikua sijiamini nilipokupigia simu kukuomba ushauri uliniambia kua nisome Kitabu chako kwanza. Nilipokisoma tu kusema kweli sikuhitaji tena ushauri wako, nilikilewa vizuri.

Niliona namna ambavyo nilikua naharibu ndoa yangu na kumlazimisha mume wangu kuchepuka. Kweli Kaka jinsi nilivyokua namnyima amani nyumbani ndiyo jinsi nilikua namfanya awe bize kazini, atumie muda mwingi huko na kuchelewa kurudi, yaani kama ulivyosema katika Kitabu chako ulikua ni mzunguko wa mume wangu anachelewa kurudi nyumbani nayeye kusema mke wangu ana kelele bora nichelewa kurudi nyumbani.

Ingawa ilikua ngumu lakini nilifuata ushuari wa Kitabu chako, niliamua kubadilika mimi na kuacha maneno. Kila wakati nilipotaka kumshutumu mume wangu na kumkasirikia yule Dada nilikumbuka katika Kitabu chako uliposema “Umeolewa wewe jiamini” kweli Kaka nilianza kujiamini na sasa nashukuru kusema kuwa nina furaha na mume wangu anafuraha anawahi kurudi nyumbani kila wakati.

Lakini sasa hivi kaka nina tatizo jingine, nipo tu nyumbani, Mungu hajanijaalia kupata ujauzito hivyo hata Dada wakazi sina, naboreka sana kukaa myewe hivyo natafuta kitu cha kufanya kujiajiri kwani ajira siku hizi hakuna. Naomba ushuari wako ni biashara gani naweza kufanya kwani nataka nikienda kumuambia mume wangu nataka kufanya kazi niwe na wazo la biashara kabisa.

No comments:

Powered by Blogger.