BAKI NA SHETANI WAKO ACHANA NA SHETANI WA MWINGINE!
Unaachana na mume wako kwakua ni malaya unaenda kutembea na mume wa mtu ukidhani kuwa anajali labda yeye ni tofauti. Dada yangu, najau kakudanganya kuwa mke wake ana matatizo, hapatani na ndugu zake.
Kakudanganya kuwa mke wake ni mchawi, hataki kufanya kazi, anamsumbua, kakupeleka mpaka kwa ndugu zake, nao wamekudhihirishia kuwa huyo mwanamke hawamtaki kwakua sijui ana nini, ila nikuambia, ukiona mume wa mtu anakutongoza basi jua kuwa hana tofauti na yule wakwako uliomuacha ndani kwakua ni malaya.
Hata mume wako akitongoza anakupondea wewe kama huyo mume wa mtu unayemuona yuko tofauti anavyomponde mke wake na maahadi kibao. Kuliko kumuacha mume wako kwasababu ni malaya ukaenda kwa mume wa mtu basi baki na huyo malaya wako tu, kila mtu abaki na shetani wake basi, ila huyo mume wa mtu atakuja kukuliza tu.
No comments: