USIMUITE MUMEO AU MWANAUME MBWA, IPO SIKU HIYO MBWA ITAPATA MFUGAJI MWEMA UTAITAFUTA HUTOIONA MILELE
Dada na mama zangu kama umebahatika kupata mume mwema ukaolewa mshukuru Mungu sana na mheshimu sana mume wako. Yabebe mapungufu yake kwa moyo wa upendo, zidisha kumuombea. Taasisi na utume mtakatifu wa Ndoa na uheshimiwe kote duniani.
Ukiwa umebahatika kuolewa wakati mwingine unaweza kumzoea mume na hata ukaona ni kitu cha kawaida sana. Dada zangu mume si kitu cha kawaida ukitaka kufahamu kuwa mume ni mali adimu ni bidhaa adimu, ni kiumbe adimu waulize wanawake ambao hawajaolewa na hususani single mothers watakueleza. Wanaweza wakawaponda wanaume kuwa ni mbwa tu lakini UKWELI MCHUNGU unawasuta na kuwashuhudia mioyoni mwao kuwa mume ni zaidi ya Tanzanite! Kumbuka hapa nazungumzia "MUME" sizungumzii wanaume iko tofauti!
Wewe mwanamke unaposema sijui hii mbwa nilikutana nayo wapi hadi ikanioa au ikawa mpenzi wangu, kuna mwanamke tena mrembo kukushinda mahali fulani naye anafunga na kuomba ili kumpata mume! Wewe endelea kumuita mbwa, ipo siku hiyo mbwa yako itampata mfugaji mwema anayejua thamani ya mbwa! Ukisema cha nini, wenzako wanasema tutampata vipi, wapi na lini?
Wanawake hawa wanasema hawajali umri, pesa, sura, wadhifa bora UHAI tu! Yani hawa wanawake wao hawahitaji utume na yakutolea, hawahitaji utume nauli, hawahitaji chochote cha kwako isipokuwa wanahitaji uwepo na upendo wako tu!
Nabii Isaya alishayatabiri haya tangu zamani za mitume na manabii katika Isaya 4:1
Ndugu zangu kinadada msiikimbie hii post ndio UKWELI MCHUNGU na hali halisi ya maisha, ukibisha ni kiburi tu na ukikataa haibadili UKWELI!
Sauti ya wasio na sauti
No comments: