Header Ads

USIVUMILIE UJINGA KWENYE MAHUSIANO ACHA KABLA YA KUACHWA



Neno UVUMILIVU lisitumike vibaya kiasi cha kuharibu mfumo wako wa maisha.. Kuna mengine hayavumiliki zaid ya mara moja.. Kuna tabia zenye kuumiza na kukera unapo vumilia unafuga ubovu
Ukiona mtu mpenz au rafiiki yako havumiliki kwa tabia zake usiogope kukaa nae mbali..
Huwezi vumillia kupigwa au kutukanwa hadharani...
Huwez vumilia mpenz kukusaliti zaid ya mara 2 zote anasema shetani alimpitia tu
Huwezi endelea kuvumilia mtu asiye kuheshimu wala kukusikiliza hata mambo ya msingi
Kumbuka
Siku zote anae penda na kujali sana ktk mahusiano ndiye anae ishia kuumia. Wanasema mwenye upendo wa DHATI hana BAHATI...Una weza mpenda sana mtu nae akajua ila yeye atapuuza hisia zako na kwenda kwa mwingine au kukusumbua makusudi akiamin kuwa huwez muacha
Anapo taka kuachana nawe kamwe usimlazimishe abak kwako. Kuna wakat bado una muhitaj ila yeye ameamua kuachana nawe huenda amempata bora zaid yako au amechoshwa na tabia zako.muache aende huwez zuia mafuriko
Inauma kuachwa na unae mpenda.lakin yapokee maumivu leo ili kesho uishi kwa furaha na aman pasipo yeye. Ukilazimisha abak kwako wakat yeye anataka kuondoka kesho atakuumiza zaid ns kusema wewe ndo umemulazimisha kubak
Kama ulishamuwekea malengo ngumu sana kumtoa akilin mwako ila utalazimika ufanye hivyo kwa faida yako... Amin kuwa yeye sio MWANAUME au MWANAMKE pekee duniani.. Kuna sehem yupo kwa ajili yako ndiye atae kuwa furaha na faraja yako
Uzur wake au pesa zake zisikufanye umlilie anapo taka kukuacha. Hapo ulipo bado unayo nafas kumpata atakae ogopa kukupoteza. Hukuwa ktk malengo yake ila yupo atakae timiza ndoto zako kuitwa BABA au MUME ama MKE.
Hakuzaliwa kwa ajili yako..yupo wako huenda nae analia na kuumizwa kama ww..mda utafika mtakutana na kuanzisha safar kisha kuishi pamoja
Usiogope kupenda kisa unakidonda cha mapenzi
Usiogope kupendwa kisa umetendwa
Unapo yasusa mapenz yy ana wapenz kwa nini ujitese kisa yeye?
Kuachana nae sio mwisho wa maisha bado utabak yule yule
Kwa nn uendelee kulia ikiwa yy kule aliko ana furaha??. Akikuona una lia na kukonda unampa jeur ya kusema yeye ndo alikuwa Nyota yako kupendeza na kufurah.. Ila akikuona una furaha na kupendeza ataumia huku akitaka jua kwa nn uwe na aman baada ya kuachana.. Mfanye ndugu na jamaa wamumcheke kukuacha mtu bora kama wewe.. Fanikisha mambo yako taarifa zitamfikia tu
Mapenz kama mchezo wa kubashiri..usiogope kuufungua moyo wako kwa mtu mwingine..huenda wa sasa ndiye utaishi nae... Hebu sasa
Jikubali
Jiamini
Jithamini
Acha kuwa mtumwa
Bado unayo nafas kujaribu tena

No comments:

Powered by Blogger.