NINGEKUA MWANAMKE NINGEMSIKILIZA MAMA ANNA
Anna alirudi kwa Mama yake, ndoa imemshinda kwakua mume wake alikua amezaa kabla ya ndoa hivyo kuna mwanamke anamsumbua sana. kila siku wanagombana na anahisi kuwa mume wake anamsikiliza zaidi huyo mwanamke. Mama yake alimsikiliza sana kisha akacheka akamuambia “Mwanangu, ukiwa ndani mwisho akirusha mawe hufungui mlango na kuanza kumrushia mawe, kwani asipoingia yeye mawe yataingia ndani.”
Anna hakuelewa, alimuuliza Mama yake alikua akimaanisha nini. Mama yake alimuambia, mwizi akija kwako lengo lake ni kuiba, anaporudha mawe kwenye nyumba yako, badala ya kufungua malango ili na wewe umrushie mawe unatakiwa kuziba mlango vizuri, kama una meza unaisi9mamisha inaziba mlango, kama una kochi unasogeza mlangoni.
Lakini ukifungua mlango ili kumpiga naye mawe yeye yuko nnje, kuna mawe mwengi ni ngumu kumzidi na hata ukimzidi basi yeye ana pakukimbilia ila wewe huwezi kuikimbia nyumba yako.” Bado hakuelewa, alishangaa ni kwanini kamuambia Mama yake kuhusu ndoa yeye analeta mambo ya nyumba ndiyo Mama yake alimuambia.
Nyumba ni ndoa yako na mwizi ni huyo mwanamke anayekutukana, yeye kwanza kazaa na mume wako, hajatosheka, anataka kuiiba ndoa yako. Ili yeye kuiharibua ndoa yako anaanza kurusha mawe ambayo ni matusi, simu za usiku, kumpost mtoto, kila kijua mume yko nyumbani katulia anapiga simu, akienda kumsalimia mtoto atapost.
Hayo ndiyo mawe, anayarusha ili ukasirike, ufungue mlango uanze kumrushia, nataka umtukane, anataka umjibu, anataka usiwe na amani, anataka umlalamikie mume wako. unapokua na kisirani, kama kila siku mnagombana mume wako atakasirika. Sasa iko hivi, kama kila siku unamsumbua mume wako kuhusu yeye na yeye anamsumbua mume wako kuhusu wewe basi jua mume wako kama mlango atachoka.
Uzuri kwake nikuwa hana ndoa, hivyo hata mume wako akiwachoka wote na kuamua kuwablock au kuwapuuza kwa kelele zenu yeye hatakua na chakupoteza, ataondoka na kwenda kwa mwanaume mwingine. Lakini wewe mumeo akikuchoka ndoa imekufa unaingia mtaani mumeo ataoa na wewe sasa utaanza kupiga simu kulalamika kuomba matumizi. Mwanangu rudi kwako, funga mlango, weka na mameza, atakuchokonoa akiiona hufungui ili aingie atachoka na kuondoka, la sivyo mtapoteza wote.
MWISHO
No comments: